Ni siku chache tu baada yakuwa na Mgogoro uliokuwa ukimtuhumu kutoa lugha ya uchochezi siku ya Chrismass aliposhusha maneno yaliyoonekana kumtaja mkuu wa nchi tofauti na serikali inavyotaka. Kama unakumbuka vizuri, Kakobe akiungana na washirika waka aliwahi kuwa na mgogoro mwingine na serikali hadi waumini wake wakagoma huku wakimuunga mkono paster au kiongozi wao huyo mwaka 2015 wakati nchi ikiongozwa na JK
Mgogoro huo ulikuwa wa umeme wa tanesco, Tanesco ikitaka kupitisha nguzo karibu na kanisa lakini Kakobe na waumini wake wakikataa na wakiamua kupishana lindo usiku na mchana ili TANESCO wasipitishe umeme na nyaya za umeme mahali pale. Sakata hilo liliisha sasa limeanzishwa lingine huku viongozi wa dini wakikatazwa kujihusisha na siasa.
No comments:
Post a Comment