Haruna Hakizimana Niyonzima Picha Limeanza Upya::
Watoto wa mjini husema dude limeamshwa au picha limeanza! Aliyekuwa kiingo wa Young Africans Haruna Niyonzima ambaye mkataba wake unaishia July 15 mwaka huu anatarajiwa kutua jijini Dar Es Salaam kama ilivyo ada kweny club yake ya awali na inasemekana Usiku wa Jana amepiga simu ya nne mfululizo tangu kuondoka klabuni hapo akidaiwa kujiunga na wekundu wa msimbazi simba , Haruna Niyonzima bado ana uhitaji mkubwa asilimia 60% kuichezea YANGA na asilimia 40% kwenda simba yeye kuendelea kupiga simu kwa viongozi ni kuomba tuu asainishwe angalau aendelee kubakia jangwani wakati Charles Mkwasa alishatangaza kuachana nae.
Vyanzo vya habari ndani ya club hiyo vimeeleza kuhusu ombi lenye radhi kubwa kuhusu kusajilisha upya niyonzima ambae mpaka dakika ya sasa hajasaini timu yoyote japo wekundu wa msimbazi wanamnyatia, Lakin inadhiirisha wadhi kwamba haitaji kushiriki ligi kuu akiwa ndani ya Simba SC kama anavyohusishwa.
Tumezungumza na moja ya kiongozi wa Young Africans kamati ya usajili kuhusiana na ujio wa niyonzima kesho wamesema nikweli niyonzima alipiga simu Jana kutoa taarifa kuwa atawasili nchini kwakuwa mkataba wake unaishia siku ya jumamosi laki lengo lake ameomba kujiunga tena na YANGA kwa msimu mpya endapo tuu atasainishwa , Lakin sisi kama viongizi wa kamati ya usajili tunasubiri maamuzi ya mwisho kutoka kwa katibu mkuu ambaye alishatangaza kuachana na niyonzima rasmi, ndio maana tunasema uhakika wa kucheza YANGA ni 60% na 40% ni za kucheza simba hivyo mpaka kufikia kesho mambo yote yatakuwa wazi pindi tuu atakapowasili na kufikia makubaliano na C. B. Mkwasa.
Pia Inasemekana niyonzima aliweza kufuatilia mazoezi yanayoendelea ndani ya club yake hapo Jana baada ya kuona clip hiyo yotube na kuzungumza na baaadhi wa wachezaji hao akiwemo Kelvin Yondan beki wa kati wa YANGA ambae nae alikua kwenye mazoezi na kumwambia kuwa anatamani tena kuendelea kucheza Young Africans endapo tuu viongozi watamuamini na kumpa nafasi!!
Source EFM SPORTS:
No comments:
Post a Comment