Mheshimiwa tundu lisu Lisu baada ya matibabu ya awali nchini kenya anatalajia kuondoka kuelekea Moja kati ya nchi za ulaya kwaajili ya matibabu zaidi. Taarifa hii imetolewa na mwenyekiti wa chama cha democrasia na maendeleo Freeman Mbowe wakati akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.
Mbowe ameeleza kuwa tarehe ya kumpeleka Ulaya ni 06 January 2018. ameongea hayo 31/12/2017 yakiwa yamesalia masaakadha ili kuufikia mwaka mpya wa 2018. Amesisitiza pia kuwa hawezi kutaja ni nchi gani atakayopelekwa kwa sababu za usalama kama anavyosema Mheshimiwa Freeman Mbowe. Msomaji wa Deepenhabari Tundu lisu alijeruhiwa akiwa anatoka bungeni na hadi sasa alikuwa hajatembea ingawa aliweza kusimama kwa miguu yake kwa mala ya kwanza akisaidiwa na madakitari wanaomtibu.
Mbowe amesema pia kua kiasi cha dollar za kimarekani 300,000 ambazo ni sawa na zaidi ya shilling 600 millions zimeshatumika kwa matibabu hadi sasa. Ameongezapia kuwa Ulaya anaenda kwaajili ya mazowezi tu na si vinginevyo.
No comments:
Post a Comment