TFF yatoa tamko juu ya Benno Kakolanya - deepentz

Breaking News

test banner
TFF yatoa tamko juu ya Benno Kakolanya

TFF yatoa tamko juu ya Benno Kakolanya

Share This
Uongozi wa Yanga umetoa ufafanuzi juu ya kukosekana kwa mlinda lango Benno Kakolanya kuwa aliomba ruhusa kwenda kumuuguza mama yake.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo Makao Makuu ya klabu ya Yanga jijini Dar es salaam, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Dismas Ten amesema uongozi wa Yanga ulimpa ruhusa Kakolanya na wamekuwa wakiwasiliana nae mara kwa mara.
Aidha Ten amevitaka vyombo vya habari kuacha kupotosha baadhi ya mambo kwani wanashusha morari ya wachezaji.
Ten amekiri kuwa ni kweli Kakolanya ana madai yake kwa uongozi na si yeye peke yake mwenye madai lakini Yanga imekuwa na utaratibu wa kushughulikia madai ya wachezaji wake.
Amesisitiza sio kweli kwamba ameondoka Yanga kwa kuwa hajalipwa pesa anazodai, bali ameondoka kwenda kumuuguza mama yake.
Kuhusu swala la Obrey Chirwa, Ten amesema Mzambia huyo naye alipewa ruhusa kwenda kwao Zambia kushughulikia matatizo ya kifamilia na anatarajiwa kurejea leo.
Ten amesema Chirwa amewasiliana na Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Yanga Hussein Nyika na amemuhakikishia kuwa atarejea leo Ijumaa.

Akizungumzia kikosi cha Yanga kilicho mkoani Mwanza kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Mbao FC, Ten amesema kikosi cha wachezaji 20 na benchi la ufundi wamefika salama jijini Mwanza.
Amesema leo watafanya mazoezi katika uwanja wa Aliance na kesho Jumamosi watatumia uwanja wa CCM Kirumba kama sheria zinavyoelekeza.
Baada ya mchezo huo utakaopigwa Jumapili, Disemba 31, Kikosi cha Yanga kitaondoka Jumatatu asubuhi kuelekea visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi.
Ten amesema Yanga imeamua kupeleka kikosi chake kamili ili kuhakikisha inafanya vizuri na hata kutwaa ubingwa.
Wakati huo huo Ten amesema Yanga inatarajiwa kutuma majina ya wachezaji watakaoshiriki michuano ya klabu bingwa barani Afrika keshokutwa Disemba 31.
Nae Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kwenye dimba la CCM Kirumba keshokutwa kuipa sapoti Yanga.
Mkwasa amesema wanafahamu Mbao FC inatafuta umaarufu kupitia Yanga hivyo siku ya Jumapili ni fursa kwa mashabiki kufika kwa wingi kuishuhudia Yanga ikidhihirisha kwa nini ni mabingwa wa Kihistoria Tanzania.
Kuhusu swala la uwanja wa Kaunda, Mkwasa amesema umwagaji wa kifusi umefanikiwa kwa kiasi kikubwa na pengine huenda zoezi hilo likafikia tamati siku chache zijazo.
Amesema dhamira ya Yanga ni kuhakikisha uwanja huo unakamilika mapema zaidi ili pengine uanze kutumika kuanzia msimu ujao.
Aidha ameitaka Idara ya Mazingira ya jiji kuhakikisha mtaro unaojengwa ukipitia karibu ya uwanja umaliziwe kwani umekuwa ukimwaga maji machafu uwanjani.
Mkwasa amesema walipeleka malalamiko yao kwa wahusika lakini wamekuwa wazito kuchukua hatua.
Amesema kama malalamiko hayo hayatafanyiwa kazi basi Yanga inaweza kufuata taratibu za kisheria.

No comments:

Post a Comment

Featured Post

ZARI alichokifanya kwa Mtoto wa DIAMOND: kamfanyia kitendo kikubbwa.

Video hii hapa chini itakujuza zaidi kuhusiana na kisa na mkasa wa alichokiaandika zari kwa mtoto huyo hii hapa  https://youtu.be/iSLPB33Mf...

Post Bottom Ad

DEEPEN TZ

Pages