Timu ya wekundu wa msimbazi imeishushia kipigo kinono timu ya Ndanda wakati wakicheza mechi yao tare 30/12/2017. Ndanda haikupata nafasi ya kufunga na badala yake imenyeshewa mvua ya magoli mawili kwa nunge 2-0. magoli hayo mawili yametoka katika timu ya Simba huku wakiwa wanamaliza mwaka 2017 vizuri kabisa maana kwao imekua shangwe kubwa katika michuwano hii ya ligi kuu VPL Tanzania bara.
Mechi hiyo ilichezwa na magoli yote mawili yakifungwa na mchezaji mahili JOHN BOCCO dakika ya 52 na dakika ya 56. Na baada ya ushindi huo mkubwa Mchezaji Haruna Niyonzima kutoka Rwanda ameweza kusifia mchezo na kiwango cha BOCCO.
Simba imeshinda mchezo huo wakiwa chini ya Kocha Mrundi baada ya kocha wao Amog kutimuliwa na kuludi kwao.
Msomaji wa Deepenhabari tunakukaribisha katika blogi hii itakayokuletea habari tofautitofauti na hasa za michezo.
No comments:
Post a Comment